Kazi Yetu

Dira na Malengo

Tafakari Upya,inalenga kuelezea utunzaji wa kumbukumbu wa pamoja katika mazingira ya baada ya migogoro, ujenzi mpya, hali ya ukimbizi na kuangalia uwezekano wa kutumika mahali pengine, katika kukuza mshikamano wa kijamii. Malengo yanategemeana: kutoka katika muktadha wa kitaifa hadi muktadha wa kimataifa, na kutoka katika kiwango kidogo hadi kiwango kikubwa kitakachoweza kutumika kila mahali.

1) Kutumia nguvu ya ndani ya makavazi kujenga ujasiri, kuonyesha masimulizi sambamba, kuongeza uelewa, huruma, na hivyo kupunguza mgongano baina ya jamii, vikundi tofauti vya kijamii, kisiasa, kidini, kiuchumi na kienyeji na kuongeza uwezekano wa amani endelevu (Malengo ya maendeleo ya Dunia namba 11/16).

2) Kuunda mtandao wa ushirikiano wa usawa wa wasomi, watunza nyaraka, wanahistoria, wanaakiolojia, wasanifu, wapangaji wa mijini, wanajiografia, watendaji, mamlaka, NGOs, waelimishaji, na wadau wa jamii zinazohusiana na taasisi za kumbukumbu na maendeleo ya jamii.

3) Kuunda mtandao, utakaojikita katika kufanya mazungumzo ya kina na yenye maana na jamii. Mazungumzo haya yawe endelevu hata baada ya mradi huu, yaunganishe tafiti mbalimbali kutoka muktadha na utaalamu tofauti tofauti utakaounganisha/kuweka pamoja hali tofauti za kisiasa ambapo mahitaji ya fikra mpya ni ya haraka. hii ni pamoja na Kambi za wakimbizi na nchi za ODA kama Tanzania, Lebanon, Ghana, Afrika Kusini na Syria.

4) Kuunda na kufanya maeneo ya kumbukumbu yawe kama sehemu ya majadiliano, kushirikisha jamii na vikundi vilivyotengwa, kuongeza na kusambaza mbinu za usomaji wa makavazi kwa undani, kubadilisha uelewa wa aina moja na kuhoji masimulizi ya aina moja na ya tofauti, kwa kuleta masimulizi ya tofauti na kuweka wazi makavazi kama matokeo ya historia nyingi na maisha ya upatanishi.

5) Kuendeleza na kuwezesha uundaji wa sehemu halisi za makavazi kama maoni ya njia ya utunzaji wake, na urithi unaohusiana (Malengo ya maendeleo ya Dunia namba 10 / 11.4), kama njia endelevu ya pamoja na makavazi ya jamii ya Baadaye.

6) kuandaa miongozo ya utendaji kwenye maeneo nyeti, kwa kuamsha makavazi yaliyopo na kuanzisha mapya, ushiriki, uhifadhi, usambazaji na ufikiaji wake. Hii itatetea jukumu la kitamaduni katika kujenga jamii zilizo na amani, zenye umoja na utambulisho wake rasmi kama hitaji la kibinadamu.

7) Kuzalisha makabrasha /maandiko ya sera na miongozo ya maadili, kwa matumizi na usimamizi wa makavazi ya baadaye. Makabrasha haya yatatumiwa pia na mashirika ya kimataifa kama OSCE, ICCROM, na UNESCO, kuhakikisha kuwa uhifadhi wa makavazi hautumiki kwa vitendo vya uingiliaji, kunyima uwezeshaji au udhibiti. Badala yake,iongoze mashirika kutumia majukwaa yao, kuelimisha na kubadili mawazo juu ya umuhimu wa mashirika makuu ya serikali, na taasisi zisizo za kiserikali na taasisi zinzazojihusisha na makumbusho.

8) Kuweka usuluhisho wa njia tofauti za uzani wa kati ili kushirikishana njia mpya za kuhifadhi makavazi. Mbinu na njia za uhifadhi za mradi huu zitatumika kama majaribio na mifano.

9) Kuweka wazi athari za ukoloni, za kimagharibi, za mfumo dume – zinazotokana na historia, na kuhifadhiwa kwa namna mbalimbali katika makavazi (kama vile video au kwa maandishi, katika kutunga na kuandaa sera.

10) Kuongeza mwingiliano wa watu na mawazo, kupitia mtandao wetu, kutengeneza daraja na ushirikiano kati ya Mashariki ya Kati na Afrika(Malengo ya maendeleo ya Dunia namba 17.14 / 17), na kwa kila: 1) kuokoa jamii katika maeneo yenye migogoro na machafuko na baada ya ukoloni; 2) jamii na mashirika, na makampuni katika muktadha wa ukimbizi; 3) watafiti katika muktadha wa kibinadamu, na idara nyingine kama, usanifu majengo, mipango-miji, watendaji walio katika taasisi za makumbusho na watunza makavazi ;4) serikali na mashirika yake

11) Kutoa mwongozo wa misaada ya kimataifa na uwekezaji juu ya umuhimu wa kufaidika na kuchota maarifa na utendaji wa wanufaika. Kuhakikisha uwepo wa mipango ya makusudi inayohusu maeneo nyeti ili isichochee chuki wala machafuko kwa kuharibu uhusiano kati ya urithi wa jamii unaoneka na usionekana.

12) Kushinikiza uwezo wa ubinadamu kwa kuiwakilisha kupitia uoanishi na usanifu, mipango miji, na makumbusho.

Njia za Kufikia Malengo

Faida za kisera na kiitifaki

Kuongeza uwezekano wa mabadiliko,ilani itaundwa na matokeo ya mradi juu ya namna ya uhifadhi wa makavazi wa pamoja. Ilani hii itakaguliwa na timu yetu na kuboreshwa wakati wote wa mradi na kusambazwa kupitia mtandao wa washiriki, taasisi za makumbusho na makavazi na kumbukumbu. Itaundwa na wadau kwaajili ya wadau, kwa ushirikiano na mamlaka zinazohusika, ambao watashiriki umiliki wa mchakato na jukumu la kutekeleza matokeo yake. Ilani hii itakuwa katika mfumo wa hati ya sera (katika lugha husika, kama Kiarabu, Akan, Kiswahili na lahaja asili), na itapatikana kwa umma wote kwenye wavuti yetu.
Itawasilishwa kwa pamoja na vitu vya kuweka kwenye makumbusho au makavazi, vinavyoonekana na visivyoonekana, kumbukumbu za video na rekodi zingine.
Kwakutumia mtandao wetu pamoja na washirika wake pamoja na mafanikio na matokeo yake chanya katika uundaji wa sera, tutayashirikisha mashirika husika kwa kuwaalika kwenye matukio na mikutano ya awali, vikao maalum vya mpangokazi, na kwa kuonyesha matokeo ya matukio haya kwenye majukwaa yao (kama OSCE, ICCROM, UNESCO). Pia tutashirikiana na timu ya GCRF na mashirika kama Makumbusho ya Uingereza, Maktaba ya Uingereza, Baraza la Uingereza na BIRI, ambao wana utaalam katika masuala ya tamaduni, urithi, maendeleo, ujenzi wa amani na sera. Tutaainisha aina ya itifaki katika kulenga njia ambazo hufanya hivyo, na namna ambavyo matokeo yetu yanapaswa kutolewa. Shabaha yetu ni kupanua maana na thamani juu ya uhifadhi wa makavazi na urithi, kwa mashirika makuu ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na taasisi za makumbusho, na hivyo kuchangia katika kutetea utamaduni kutambuliwa, kwa kiwango rasmi, kama hitaji la kibinadamu na haki (Malengo ya Maendeleo Dunia SDG 11.4).

Kuunda Mtandao wa Ushirikiano wa pamoja na kuunganisha maeneo.

Ushirikiano wa ndani utaimarishwa kupitia ushirikiano mpya, kuwezesha upatikanaji wa kumbukumbu na masimulizi, na sehemu yake katika muktadha wa hali ya juu. Hii itakuwa kupitia warsha, kutembelea maeneo ya kumbukumbu, kuunda na kutathmini njia za pamoja na upimaji wa teknolojia mpya. Kufanya kazi kupitia mtandao kutaimarisha maombi ya pamoja ya upatikanaji wa kumbukumbu, ikiruhusu nafasi nyeti na yenye nguvu katika mashauriano na mazungumzo ya jamii na serikali (mfano Abasia ya Wabenediktini Tanzania, alijiunga kama washirika ili kufanya kazi katika kuhakikisha upatikanaji huu). Exeter, itawashirikisha wanaomtandao rasilimali zake kwa kuanzisha nafasi za heshima na ukuzaji katika taasisi nyingi.
Tunashiriki na kusaidia mipango ya washirika ya kujenga uwezo kama maabara ya AUB’s huko Lebanoni, kwa kuwezesha mazungumzo na maabara za Baddawi, Syrbanism na London Urban Lab. Katika Kambi ya Baddawi, tutavijengea uwezo vikundi hai vya vijana katika Klabu zao za Utamaduni, kupitia shughuli za ujumuishaji na warsha ya maabara ya Tanzania na warsha za teknolojia zitzakazosaidiwa na zana za kazi na, utaalamu kutoka CSM (London) na LDRC (Legon). Shughuli hizi zinazounganisha maeneo zitatoa fursa kwa washiriki kuchangamana na kuunganisha kwa wakati na nafasi, kupitia kile kinachoweza kujulikana kama makavazi ya pamoja ambayo ni ya wote. Uoanishaji wa masilahi ya kiutafiti na Taasisi za kihistoria, maumivu/machungu na mabadiliko ya Stellenbosch (SA), imeanza kuangalia uwezekano wa kuanzisha kituo cha uchunguzi wa pamoja kutafuta njia mpya za kuweka kumbukumbu (angalia barua ya Gobodo-Madikizela). Maswala ya kijumuishi juu ya kumbukumbu na uhifadhi wa data yamejitokeza pia katika mazungumzo na jamii ya Lindi, SMUC huko Mtwara, na LDRC huko Legon. Ziara yetu ya majaribio nchini Tanzania iliweza kuchochea hali hii. Uhifadhi wa kavazi zisizo za jadi ni muhimu kwa kazi ya Siria mjini, ambayo itaimarisha zana za ujenzi wa maendeleo ya miji ili kuongeza ujumuishaji wa kijamii, heshima kwa haki za binadamu na haki za kumiliki mali. Mfumo wa mradi umeundwa kuchochea maingiliano haya ya washirika, kuimarisha uwezo wa ubadilishanaji wa maarifa, usambazaji wake, ujenzi wa mbinu na ushirikiano.

Kuokoa na Kuhifadhi masimulizi kupitia Mifano ya maeneo maalum na Ushirikishwaji wa makavazi

Kukutana na watafiti uwandani, jamii na maofisa wengine italeta/itavutia mwitikio wa wadau wenye uzoefu juu ya mizozo, ukoloni, ukimbizi na juhudi za kuboresha. Mikutano hii itarekodiwa kwa kufuata taratibu na maadili na kuhifadhiwa kwa kipindi chote cha mradi. Uandaaji wa Makavazi na usambazaji (kupitia mitandao, maonyesho au uigizaji), utakuwa katika aina tofauti kama hadithi, nyimbo, dansi, vitu au uainishaji wa mandhari. Hazina ya makavazi itakuwa kwenye tovuti kama itawezekana, ili kutumiwa na wanafunzi, watafiti na umma kwa ujumla bila gharama yeyote na kwa kuzingatia muktadha wa taarifa, kwa kuangalia mbinu na mifano kutoka LDRC na CSM. Uundaji wa hazina hizi kwa maeneo yasiyonayo, utawezeshwa kupitia mapendekezo yaliyoandaliwa na timu ya mradi na wadau wengine. Watachochea majadiliano ya nini kinaweza kuwekwa kumbukumbu kutoka makazi yao (au diaspora), na ni kwa namna gani zinahusiana na ‘maeneo’ yao. Kupitia shughuli hizi tunategemea kuwa na faida zifuatayo: kuboresha masimulizi mseto ya kihistoria kwa kuonyesha sauti changamani, kufundishia, utalii na kuhuisha tena mandhari ya kumbukumbu. Tunatambua changamoto za kuonyesha hadithi mseto, hasa za vikundi vilivyotengwa, kwa hivyo kwa mara ya kwanza uamuzi wa pamoja utafanywa kwa kushauriana na vikundi hivi juu ya rekodi, uhifadhi na ufikiaji. Tunaamini kuwa mchakato pekee wa kuweka kumbukumbu, hata ikiwa matokeo yake hayatatolewa kwa umma utsababisha kujiamini na wakala wa utambuzi wa thamani ya masimulizi husika.

Kuhuisha maeneo ya Kumbukumbu – Makavazi na Mazingira yasiyokuwa na Makavazi

Wakati wa shughuli za maabara tuatashughulikia/tutafuta na kukomesha uandishi wa kutia chumvi ukiwa umehamasishwa au tutengenezwa. Itaonyesha mtazamo ambao simulizi huwekwa katika mazingira, ya kukumbukwa au yasiyokumbukwa – yaliyojengwa na yasiyojengwa: liwe Jiji au Kambi-kama-makavazi ya huko Beirut au Baddawi, au mazingira ya biashara na vita nchini Tanzania na Ghana. Faida zake zitakuwa kubwa katika mchakato wa uhuishaji na ujenzi mpya. Uchunguzi wetu unadhihirisha/bainisha udhaifu na usumbufu, ukimbizi na kutengwa, na hivyo kufanya kazi kwa kuunda pamoja aina mpya ya uelewaji wa mazingira ya kumbukumbu, na maoni ya uhuishaji pale inapohitajika na kuwezekana kwa kuchora ramani za maeneo ya kumbukumbu (kama vile. Gereza la zamani, Lindi au Beit Beirut). Kusudi la hatua hizi ni kuchangia katika kuzaliwa upya miji na mikoa, kuhamasisha kuongeza nafasi za majadiliano na kujifunza kwa pamoja fursa na ushiriki unaofaidisha umma. Umakini katika uhuishaji wa maeneo haya utaongeza nguvu ya ilani yetu katika kubadili tabia ya mashirika ya kutunga sera na kuwekeza katika kupanga na ujenzi ili kuhakikisha kuwa wanakuwa makini katika utunzaji wa makavazi wa pamoja. Hii ni kwa kuchunguza jinsi mazingira yanavyoathiri wale wanaokimbia makazi yao – jinsi mtu ‘anavyoweza kuandika kutoka ndani ya kambi’ (jina la kazi ya Qasmiyeh) – tunakusudia kutumia maoni ya watu wanaoishi kwenye maeneo ya ukimbizi, dhima na uzoefu wa maeneo hayo, kuonyesha jinsi zilivyo jumuishwa na kupanua maana ya makazi ya ulimwengu. Ikiwa itatafakariwa tena maeneo ya zamani au ya sasa na maisha kutoka mbali, uchambuzi utafuatilia uhusiano kati ya (kabla ya) ukoloni, kuwekwa kizuizini, wakimbizi na makazi/watu au makambi ya kulazimishwa ukichunguza njia ambazo kwa aina hiyo ya ushiriki inaweza kuleta (halisi na dhahania) maisha na masimulizi zaidi ya mipaka ya kambi za wakimbizi.

Kujenga Uwezo wa muda mrefu wa Makavazi binafsi na Utafiti

Kuwezesha majadiliano juu ya uhifadhi wa kumbukumbu na pia kuwezesha majaribio ya aina za makavazi, mradi huu utaandaa njia ambayo moja kwa moja itatokana na njia za jadi, mbinu za kiteknolojia na za kitafiti za kisasa juu ya utafiti wa makavazi yanayotegemea jamii. Tunachanganya makavazi na timu pamoja na uhifadhi nyara-binafsi, kama tulivyofanya kwa mradi wa majaribio Tanzania ambayo matokeo yake yalitoa kumbukumbu za simulizi katika muktadha wa filamu (toleo fupi tayari limesambazwa kwa wadau, na kwenye wavuti yetu ya mradi). Pamoja na hilo, mkusanyiko wa hadithi, mashairi, michezo, densi kuhusu vita vya Majimaji, iliyoandaliwa na wanafunzi wa shule na kuwekwa katika kijitabu kitakachosambazwa mikoani na katika mashule kuonyesha uelewa wa aina mbalimbali wa vita hii. Kijitabu hiki kinajumuisha muhtasari wa matokeo ya hivi karibuni ya kihistoria na ya akiolojia kuhusu vita vya Majimaji kutoka kwenye utafiti wa Rushohora na Silayo. Mchakato wa uundaji wa makavazi hii na matokeo yake yanaonyesha namna mbinu mbadala zinavyofanya kazi katika jamii. Kuongeza uwezo wa uchunguzi katika siku za usoni kupitia uwekaji makavazi wa binafsi, ili kuboresha masimulizi, wataalam wa mradi huu na mbinu zake, hasa kutoka CSM watawafundisha washiriki teknolojia kama upigaji picha, suluhisho la data rununu kama Raspberry Pi, na njia za kuweka makavazi kama Omeka na blockchain (tazama pia DMP). Warsha zimepangwa na kikundi cha vijana kinacholetwa pamoja na dijiti katika Klabu ya utamaduni kutoka kambi ya Baddawi, Palestina. Tunakusudia kuacha vifaa na kuwezesha upatikanaji wa programu, ili kuwezesha uwepo wa majaribio yanayoendelea ya njia hizi baada ya mradi. Tumejipanga pia kusaidia watu kuja kupata mafunzo katika kituo cha CSM London. Uboreshaji wa kituo cha kuhifadhi mtandao kwenye nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea (ODA na nchi zisizo za ODA) itawezesha mwendelezo wa mitandao kati ya washirika na kuwajengea uwezo wa kuweka makavazi-binafsi na kufanya utafiti. Faida zaidi ya utendaji huu ni uendelevu na ukuzaji wa ujuzi na njia za kuchukua hatua za maendeleo ya baadaye.

Kujenga Uwezo wa Taasisi ndani ya Ushirikiano

Malengo ya muda mrefu ya Mtandao ni kuongezeka kwa uwezo wa kitaasisi ndani ya ushirikiano ili kukuza na kutekeleza mbinu bora za pamoja za kufanya kazi. Hii inajumuisha kushirikiana katika kuunda mbinu na rasilimali ili kusimamia ajenda zinazohusiana na maadili, usalama, upembuzi yakinifu na usimamizi wa tahadhari, na kuhakikisha usawa na uwiano. Mtandao wa Tafakari Upya kupitia timu ya Maadili na Ripoti watafanya uhakiki yakinifu wa sera za kitaasisi zinazohusu mbinu hizizinavyofanya kazi ndani ya taasisi, na washirika wanaoshirikiana na AHRC. Kwasababu hatuwezi kuhakikishiwa kuwa taasisi zitapitisha mapendekezo yetu, tutatoa hati za mfano za kuzingatiwa (zilizorekebishwa ili kuhakikisha kuwa zinalenga muktadha), na tutasimamia matumizi yake ndani ya mradi, kwa lengo la kujenga mbinu bora. Ubunifu na uundaji wa pamoja wa maarifa, kwanza katika maabara, na piakatika mikusanyiko ambayo inaleta wadau wengine kutoka mwanzoni, itaongeza uwezekano wa ushawishi na hivyo uwezekano wa kupatikana matokeo chanya. Faida za muda mrefu za shughuli kama hii zitakuwa kuongezeka kwa maarifa na ujasiri wa taasisi zote kwa ushirikiano kufanya tafiti sahihi na za kufuata maadili na kujali muktadha hivyo kuwa uwezekano mdogo wa kupoteza hadhi na matumizi mabaya ya fedha. Hii pia itafaidisha washirika wa mradi kwa kujenga msingi wa kushirikiana katika miradi ya baadae.

Rekodi ya Mafanikio

Timu ya Mtandao huu imeonyesha rekodi ya kufanya utafiti kwa kushirikiana na washirika wa kimataifa, pamoja na tafiti zilizoongozwa na ODA. Ushirikiano huu unaangazia ushirikiano wa ukanda wa Kusini na Kusini na Kusini-Kaskazini wa ulimwengu. Matokeo ya ushirikiano huu, na mbinu zilizotumika zimeorodheshwa katika machapisho ya wajumbe wa timu (kwa mfano, Chapisho la Al-Harithy linaloitwa “Uokoaji wa Sehemu za Urithi wa Utamaduni Baada ya Vita: Aleppo Taht AlQala’a”; Kitabu cha Fiddian-Qasmiyeh cha “Mahusiano ya Kusini na Kusini”; Chapisho la Gavua linaloitwa “Siasa za Urithi barani Afrika”; chapisho jingine ni la Isayev kwa IRRC, “Uhamiaji, Uhamaji na Mahali na ‘Kati ya Ukarimu na Kimbilio” na andiko jingine ni la Rushohora “Maburi, Nyumba za Machungu na Utekelezaji wa Mauaji).
Matokeo ya sera za utafiti za wanatimu, zilizoorodheshwa katika wasifu wao, unathibitishwa kupitia mashauriano mara kwa mara na mashirika ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama UNESCO na UNHCR, OSCE, ICCROM, Benki ya Dunia, Kikundi cha sera ya kibinadamu-ODI, na Oxfam, ambayo hutoa njia za moja kwa moja za kufikia malengo na usambazaji wa matokeo ya mradi kwa watengenezaji sera, hii ni pamoja na washirika wa mradi kama Mkoa wa Lindi. Washirika wetu wa mradi wameonyesha uwezo wa kuwasilisha utafiti kwa umma kupitia media, ikiwa ni pamoja na kuandika au kazi zao kuonekana katika jarida la New York Times, BBC, The Guardian, CNN, Washington Post, Bloomberg, National Geographic, Historia, na TED , na mahojiano kuhusu makala katika vyombo mbalimbali vya ziada vya habari pamoja na maonyesho ya sanaa na mabango nchini Tanzania, Lebanon, Ghana, China, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani, Italia, na kwenye mitandao.