Maabara ya Baddawi

Wenyeji ni:

Yousif M. Qasmiyeh, Chuo Kikuu cha Oxford
Elena Fiddian-Qasmiyeh, UCL
Klabu ya kitamaduni ya Kambi ya Baddawi, Mshirika wa Mradi

Imeandikwa na kuhaririwa na:

Elena Fiddian-Qasmiyeh na Yousif M. Qasmiyeh pamoja na Timu ya Tafakari Upya

Maabara ya Baddawi inatekeleza makavazi ya pamoja kwa urekebishaji kupitia kukuza ushirika uliopo na uharibifu (Qasmiyeh 2019) na mbinu tofauti(Fiddian-Qasmiyeh 2019a / b) na kuendeleza kwenye mbinu zilizoshirikishwa na timu ya Maabara ya Tanzania. Maabara hiyo inatoa fursa ya kutafakari juu ya safu ya uhusiano wa kihistoria, kijamii na dhana kati ya Kambi ya Baddawi na baadhi ya mada na maeneo zilizochunguzwa na Timu ya Tanzania, hasa kuhusu aina mbalimbali za kumbukumbu na simulizi za maeneo ya kumbukumbu.
Hii tayari imechunguzwa kufuatia ziara ya majaribio mnamo Julai 2019, na idadi ya makusanyiko na semina za ubunifu zilizopangwa kufanyika msimu wa 2020. Kwa lengo la kujenga uhusiano na maeneo ya Kitanzania, Maabara ya Baddawi itawezesha maeneo matatu (3) ya kujifunzia. Haya yatakuwa kama vichocheo vya ujenzi wa mbinu yetu na njia ya muktadha wa msingi wa uhifadhi wa makavazi ya pamoja na kupima uhamishaji wake katika maeneo na nyakati.

1: Kusafiri na uharibifu uliokomaa katika magereza ya kikoloni nchini Tanzania na UNRWA na PLO na malazi hatarishi katika Kambi ya Baddawi. Kupitia mahojiano, masimulizi ya kihistoria (maarufu na ya kitaasisi) uchambuzi wa makavazi, uandishi wa ubunifu, na picha; kesi hii itachunguza urith wa zamani, wa sasa na wa baadaye wa makazi ya bomu ya UNRWA na PLO katika Kambi ya Baddawi, kuyaweka kwenye mazungumzo na uchambuzi wa timu juu ya magereza ya kikoloni nchini Tanzania. Tunavutiwa sana na jinsi maeneo haya (malazi na magereza) zimebadilishwa kuwa mahali pa uharibifu ambapo zamani na sasa zinakutana mara kwa mara na kupishana wakati wanatafakari hatma yao. Wakati wa miaka ya 1970-90s (kwa kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara ya anga ya Israeli na Palestina, Lebanon na Syria), shule za Baddawi UNRWA zilikuwa na makazi ya binafsi ya mabomu.
Hizi ziliharibiwa na kurudiwa tena kama msingi wa shule hizi wakati wa ujenzi uliofuata. Shule hizi mbali na mambo mengine zilitumika tena baadaye, na watu waliohamishwa kutoka kambi ya Nahr el-Bared mnamo 2007 (ambayo ilibomolewa chini na wanajeshi wa Lebanon) na kutoka Syria tangu 2011. Katika kipindi hicho hicho, PLO ilijengwa na / au kufadhili ujenzi wa makazi ya bomu kwenye kambi.
Tunasema kwamba malazi yaliyojengwa ndani ya UNRWA yalikuwa ni maeneo ambayo yalithibitisha kwamba kambi hiyo na wakaazi wake (na miradi ya kisiasa) walikuwa kwenye tishio la shambulio lisilopingika, na baadaye yalibomolewa na UNRWA kama njia ya kukomesha matarajio ya kushambuliwa na ‘kufifisha’ hali ya kisiasa kwenye kambi. Kupitia uharibifu huo, makazi hatarishi ya UNRWA yametoa misingi halisi kwa shule ambazo zimefundisha vikundi tofauti vya watoto waliohamishwa, na hivyo kuendelea kuchukua jukumu muhimu katika ‘tafakari upya’ za kizazi cha vijana wanaoishi katika Kambi ya Baddawi.

Kwa kulinganisha, makazi ya mabomu ya PLO – ambayo funguo zake zinashikiliwa na Kamati Maarufu ya kambi hiyo – inabaki kama maeneo ya ‘miungu’ ambayo yako kambini. Kwa kuwa imekuwa haiwezekani (kwa sababu za kisiasa na kimiundombinu) kubomoa na kuziunda upya, za kale, sasa na baadaye, makazi haya bado hayajashughulikiwa hadi sasa.

2: Kuwatafuta Waafrika wa Kipalestina na Wapalestina wa Kiafrika katika Kambi ya Baddawi. Upande wa juu wa eneo la Kambi ambapo shule za UNRWA (na kwa hivyo makazi ya mabomu) yapo pia makazi ya Ah al Mu Mujjarin: ambayo ni nyumba za Wapalestina wa asili ya Waafrika waliohamishwa (hasa kutoka kambi ya al-Nabatieh) kwenda Kambi ya Baddawi miaka ya 1970. Utafiti huu utajikita katika uhusiano wa zamani, wa sasa na (wa baadae) wa siku zijazo kati ya kambi ya Baddawi na watu tofauti tofauti na maeneo na kanda mbalimbali za Afrika.

Inasadikiwa kuwa Waafrika-Wapalestina / Wapalestina weusi ni kundi la Wapalestina ambalo halijafanyiwa utafiti sana (kwa kiasi kikubwa ni pamoja na huko Lebanon),hivyo suala hili litahakikisha kuwa kwamba maeneo tofauti ya kambi na / kama makavazi yatapewa kipaumbele cha uchambuzi wetu. Kiunganishi kingine kwa Afrika, na hasa Tanzania, ni jukumu la Tanzania katika kuwakaribisha wasomi na viongozi wa Palestina waliokuwa ukimbizini miaka ya 1960. Kesi hii itajihusisha kwa umakini na njia ambazo uhamishaji hujumuisha makazi mengine kwa kuzingatia historia zinazoingiliana.

3: Machungu/maumivu na Nafasi katika Baddawi. Suala hili linahusiana na hoja ya timu ya Tanzania iliyotokana na majaribio yao ya kwenda kwenye “shamba la pamba lililojaa machungu/maumivu (inaaminika halilimwi tena kwa sababu ya machungu/maumivu yaliyoanzia hapo)”, na inachunguza jinsi na kwa nini nafasi/maeneo mengine ya kihistoria yanayohusiana na vurugu na machungu yamekuja kuunda msingi wa kambi ya wakimbizi wa kisasa na eneo la jirani yake (Jebel al-Baddawi). Mbali na makazi hatarishi ya UNRWA na PLO, tutaangalia jinsi hali ya sintofahamu kwenye vizingiti vya kambi – kama vile misitu ya Zeitun (mizeituni), misitu ya Jebali (kilima / mlima) na viwanja vya mpira – vimebadilishwa na jumuiya ya Wapalestina na Walebanoni na kuwa nafasi/maeneo mpya ya kumbukumbu na tafakari upya.