Maabara ya Ghana

Mwenyeji ni:

Kodzo Gavua, Mkurugenzi wa Kituo cha Rasilimali za Dijiti za A.G. Leventis (Chuo Kikuu cha Ghana) 

Imeandikwa na kuhaririwa na:

Kodzo Gavua na Zonke Guddah na Timu ya Tafakari Upya

Maabara ya Ghana itachunguza njia ambazo vikundi mbalimbali vya watu vinavyopatikana kandokando mwa pwani ya Ghana vinafanya kumbukizi ya zamani na kuendelea na hali yao ya kijamii na kimazingira na kuishi kwa amani na urafiki, licha ya hali yao ya kihistoria ya ugomvi na uharibifu.
Ukanda wa pwani wa Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara ni maeneo ya mwanzo kabisa ambapo Waafrika na Wazungu walianza kuingiliana moja kwa moja na kwa kiwango kikubwa. Eneo hili lina makazi ya watu kutoka matabaka mbalimbali yanayotofautiana kiutamaduni, kihistoria na kijiografia. Punde Baada tu ya 1471 wakati wafanyabiashara wa Ureno walipoanza kuchangamana nao, watu wa eneo hili walibatilishwa na wimbi la makazi ya Wazungu pamoja na Waholanzi, Wadenishi, Wajerumani na Waingereza, hadi Ghana ilipojipatia uhuru wake 1957.
Mwingiliano kati ya vikundi mbali mbali vya watu vimekuwa na sifa ya kijeshi na aina mbalimbali za migogoro. Taasisi, maadili, na njia zingine za maisha ambazo Wazungu walianzisha na, kulazimishwa kwa watu wa eneo hili zilipingana na mila za wenyeji na kusababisha mivutano na mizozo na vurugu ya kuingiliana baina ya vikundi. Urithi wa historia hii ya pwani na njia ambazo wenyeji wanafanya mikakati na kuelekeza hali zao za maisha bado hazijaeleweka vizuri, kuhifadhiwa na kufanya zipatikane na kuhabarisha ya hatma ya watu. Katika hili tunataka kushinikiza jinsi utumwa utakavyokumbukwa katika siku zijazo, na kuiweka kama moja ya hadithi nyingi, ikibainisha tofauti na namna zinavyoingiliana
Kwa hivyo lengo letu litakuwa kutafuta na kukusanya habari juu ya jinsi watu wa pwani wanavyojipambanua na wanavyopenda kutambuliwa, mizozo mikuu ya kihistoria na na matukio wanayokumbuka kumbuka na kukumbushana, kwa nini na jinsi wanavyokumbushana na kutunza matukio hayo na jinsi wanavyoshiriki na kuungana na hali zao za zamani na kushinda hali hiyo ya mgogoro ili kuishi kwa amani. Tutaongozwa katika juhudi hii ya kiada kwamba watu wa pwani ya Ghana wana urithi wa pamoja wa kitamaduni ambao unatokana na karne nyingi za mwingiliano wa kitamaduni. Walakini, ufahamu wa kutosha wa umma, uelewa, na watu kuthaminiwa asili yao, utofauti wao na mahali pa upendeleo wa kimataifa, ugomvi wa hisia, mivutano, na migogoro.

Kazi yetu itajikita zaidi eneo la Elmina ambapo wafanyabiashara wa Ureno walikaa kwanza na ambapo jumba kongwe zaidi la kizungu barani Afrika , Kusini mwa Jangwa la Sahara lilijengwa na wafayabiashara hawa mnamo mwaka 1482 na kuitwa São Jorge da Mina. Ili kuhakikisha uwakilishi wa usawa wa hali ya pwani ya Ghana, hata hivyo, tutapanua wigo wetu kufikia maeneo mengine mawili ya pwani, Jamestown, Accra na Keta, Anlo.
Tukiongozwa na sera ya Maadili ya Chuo Kikuu cha Ghana, tutatumia njia na mbinu mchanganyiko na kutumia mchanganyiko wa ethnografia, ethnografia ya kihistoria, vyombo vya kidijiti na mikakati mingine ya utafiti wa anthropolojia kupata taarifa/data kutoka kwa vyanzo vingi, vya kawaida na vya mbadala. Kwa mfano, tutashirikiana na Idara ya Utawala wa Rekodi na Hifadhi ya Jumuiya ya Ghana (PRAAD) na tutatambua na kushirikiana na familia, viongozi wa jadi, wasimamizi wa serikali, makanisa, shule na vyama vya ushirika.

Pia tutasoma ripoti za akiolojia na kihistoria za maeneo husika, majengo, vitu na taarifa tunazoweza kupata kutoka kwenye maonyesho ya jamii ya sanaa na hadithi zingine ambazo zinaelezea na kuonyesha watu wa zamani na wa sasa. Mfumo wetu wa utafiti, ukichota kutoka kwenye uzoefu wa maabara zingine, utatuwezesha kupata habari rasmi na zisizowekwa rasmi ambazo mara nyingi huangaziwa katika utafiti wa kibinadamu, na kuchunguza mazingira yenyewe kama makavazi. Sio lengo letu basi kuchanganya hizi kuwa simulizi mpya bali kuangazia sawasawa na kuongeza aina za makavazi ambazo zinaonyesha uzoefu uliopo na makavazi ambazo zina thamani na umuhimu.