Maabara ya Tanzania

Wenyeji ni:

Nancy Rushohora, Chuo Kikuu cha Stellenbosch;
Valence Silayo, Chuo Kikuu cha Tumaini, Ndaki ya Dar es salaam.

Imeandika na Kuhaririwa na:

Nancy Rushohora na Valence Silayo pamoja na Timu ya Tafakari Upya.

Kufikia sasa tumeweza kuendesha mradi mdogo wa majaribio, uliofanyika Lindi, Tanzania, na kuoanishwa na Kambi ya Baddawi, Lebanon na Kituo Cha Mt. Martins,London, Uingereza, na kufadhiliwa na tuzo ya maendeleo ya GCRF – AHRC. Matokeo ya awali yamewekwa katika muhtasari wa filamu fupi iliyoandaliwa na Mark Kaplan ( na kuhaririwa na Nancy Rushohora na Izette Mostert) (kwa Kiingereza |kwa Kiswahili).

Maabara ya Tanzania itangalia kwa undani zaidi vita vya Majimaji. Hasa kumbukumbu za jumla za ukatili wa kikoloni kati ya kizazi na kizazi. Tofauti kati ya historia rasmi na isiyo rasmi itachunguzwa pamoja na aina na mipaka ya ushujaa – mara nyingi katika mgogoro huu wenye sura nyingi, ushujaa wa jinsia umesisitizwa zaidi. Kama sehemu ya kuchunguza na kudhihirisha simulizi tofauti tofauti, maabara itashughulikia mienendo ya kumbukumbu zilizofungwa na zilizo wazi, na namna ambavyo taarifa zilizofumbwa zinaweza kuongea kupitia njia nyingine-katika kuelezea hadithi za kutokuwepo. Maabara ya Tanzania pia ni juu ya hali, upatanishi na utunzaji wa masimulizi ya Vita vya Majimaji kwa njia ya kidijitali kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu (Rushohora 2019; Silayo 2020).
Sauti za kizazi cha 3 au 4 cha waathirika wa ukatili wa kikoloni zitasikilizwa na kurekodiwa jinsi mwingiliano na machungu/maumivu yanavyoathiri kumbukumbu kama hizo. Washirika wetu wa kitaasisi, pamoja na viongozi wa jamii kama vile Mwenye Mchekenje wa Ndanda na familia yake, ni: Monasteri ya Wabenediktini wa Ndanda, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, na Jumba la kumbukumbu ya ya Taifa, Tanzania na Makumbusho ya vita ya Mjimaji Songea.

Shughuli zinazopaswa kufanywa kupitia Maabara ya Tanzania ni pamoja na: 1) Kurekodi na kudijitisha mazungumzo. Hii itahusisha kutembelea maeneo ya kumbukumbu na kusikiliza hadithi za ukatili wa kikoloni ambazo zitawezesha utengenezaji wa filamu na udijitishaji wa makavazi. Mpango zaidi wa kitamaduni utatumia vifaa vya kitamaduni vilivyoandaliwa katika Kambi ya Baddawi na kinyume chake. 2) Tabaka za historia, kumbukumbu na uharibifu kama kumbukumbu. Miji ya pwani ya kusini mwa Tanzania inaunda tabaka la historia, kumbukumbu na uharibifu ambao unaunganisha mradi huu na maabara ya mjini, Beirut, pamoja na maabara ya Ghana ya mandhari ya pwani. Kwakutumia sauti za wanajamii, vifaa vya vinasa sauti, majengo kale na serikali tunakusudia kukuza njia za kusoma vya kale kupitia kudharau maeneo, na / au migogoro ya kimaeneo
3) Ushirikiano wa uzalishaji maarifa. Kwa kushirikiana na jamii ya eneo tunakusudia kuchunguza na kuunda kituo cha rasilimali ya dijiti ambayo inajumuisha njia rasmi na zisizo rasmi za uzalishaji wa maarifa. Kituo cha rasilimali za dijiti kitaanzishwa wakati wa awamu ya kuagiza miradi na kitahudumiwa katika Chuo Kikuu cha Tumaini ndaki ya Dar es Salaam, kituo hiki kitafuata mfano wa kituo cha rasilimali cha Leventis katika Chuo Kikuu cha Ghana (LDRC). Mfumo wa mtandaoni wa kanzi data utaratibiwa kwa pamoja na kwa kubadilishana kati ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch (Afrika Kusini) na kituo cha rasilimali cha Leventis katika Chuo Kikuu cha Ghana (LDRC)(Afrika Magharibi) kwa urahisi wa kupatikana katika bara lote.

Teknolojia ya dijiti ya utunzaji makavazi binafsi iliyoundwa tayari na washirika wengine (kama CSM, London) itapimwa katika muktadha wa makavazi za jamii kama mkakati wa nyaraka kutoka chini na pia itakuwa sehemu ya nyenzo za kufundishia. Warsha juu ya kuelewa kumbukumbu za vizazi na vizazi katika muktadha maeneo ya mazingira, magofu, mazingira na kiwewe, itaonyesha uzoefu kutoka Tanzania, Lebanon na Afrika Kusini baada ya ubaguzi wa rangi. Sehemu ya Afrika Kusini itafanywa kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Kiti cha maumivu/uchungu cha kihistoria na mabadiliko chuo Chuo Kikuu cha Stellenbosch.