Mwanzo

Tafakari Upya
Inalenga kuchangia
Kuzuia Migogoro, na Kuijenga Amani ya kudumu
Na
Kupunguza vikwazo katika kushirikiana
kwa kuunda njia za uelewa wa pamoja wa
Usawa katika utunzaji nyaraka
ikihusianishwa na
mbinu za pamoja
na kutetea
Utamaduni utambuliwe kama Hitaji la Kibinadamu

Makavazi ni majadiliano juu ya maono au dira ya siku zijazo. Makavazi yana hadithi na habari ambazo zitaendelea kusimuliwa bila kusahaulika. Ikiwapo na usahaulifu, aghalabu hukithiri baada ya migogoro, uhamisho na ujenzi wa makazi mapya. Mtandao huu wa ushirikiano wa kimataifa utaunganisha wataalamu kutoka katika muktadha ambao matukio haya yamejitokeza sana kwa mfano Lebanon, Tanzania, Ghana, Afrika Kusini, na ikibidi hata Syria.

Hapa tutaunda mbinu au njia zitakazoonesha usawa katika uhifadhi wa kumbukumbu, njia itayoruhusu uvumilivu na utambuzi wa uzoefu na simulizi nyingi za zamani ambazo zinapingana na masimulizi ya upande mmoja.

Matarajio yetu ni kufanya haya yote kwa kutumia: Maabara za uchunguzi, miradi maalum, uundaji/uandaaji wa makavazi mpya, kusoma kwa umakini kupitia makavazi zilizopo, na kupitia upya maeneo ya kumbukumbu. Kufikia sasa tumeweza kuendesha mradi mdogo wa majaribio, uliofanyika Lindi, Tanzania, na kulinganishwa na Kambi ya Baddawi huko Lebanon na Central St Martins huko London, Uingereza. Mradi huu wa majaribio ulifadhiliwa na GCRF – AHRC. Matokeo ya awali yapo katika filamu fupi inayoitwa “Tafakari upya maeneo ya kumbukumbu”. Filamu imechukuliwa na Mark Kaplan na kuhaririwa na Nancy Rushohora na Izette Mostert. (Kiingereza | Kiswahili).

HABARI/TAARIFA: Tunafurahi kuwa Baraza la Utafiti la Utu na Binadamu (AHRC) limefadhili mradi wa Kutafakari Upya Makavazi kwa kiasi cha Pauni za Uingereza milioni 2. Ufadhili huu ni sehemu ya mpango wa Mfuko wa Utafiti wa Changamoto za kimataifa (GCRF). Waraka wa taarifa umeambatanishwa hapa.

[Un]Archiving Lab Proposals

Future Commissions – Watch this Space