Tunachokifanya/Kazi Tunazofanya

Makavazi ni sehemu yenye mjadala kuhusu maono ya nyakati zijazo.
Maamuzi kuhusu nini kikusanywe, kihifadhiwe au kitumiwe mara nyingi hutokana na masimulizi ya namna juu ya wengine au masimulizi mengine. Hii ina maana kwamba ni hadithi gani iendelee kusimuliwa na ipi iachwe. Maswali haya ni ya msingi baada ya malumbano au migogoro ya kivita, kuhamishwa ama ujenzi mpya wa jamii. Mtandao wetu unaunganisha utaalam kutoka katika muktadha ambao maswala haya yametokea: mfano Lebanon, Tanzania, Ghana, Afrika Kusini, na hata Syria. Hizi ni sehemu zetu za kuanzia utafiti na kuunda mbinu za usawa za uhifadhi wa makavazi inayoruhusu matumizi ya njia mbalimbali za kuelezea matukio ya kihistoria zikihusisha mazungumzo katika vizazi, jinsia, viwango tofauti tofauti, kabila, vikundi vya hadhi na wadau mbalimbali.

Tafakari Upya, hujumuisha makavazi yalivyoandaliwa katika sauti au muktadha mbalimbali. Hii ni muhimu sana kwasababu tunajishughulisha na makavazi yanayoelezea maeneo yenye migogoro ya kivita.Tunapima njia mbadala zinazoruhusu majadiliano ya wazi na kupinga mlengo wa njia moja. Tunalenga utunzaji makavazi unaochota kutoka kwenye maarifa za jamii husika na kuipa jamii mamlaka ya kipekee katika kufikia maamuzi ya pamoja juu ya kitu gani kikumbukwe au kisahaulike. Mbinu hizi zinapinga mijadala, uboreshaji, ubaguzi, na kutokuthaminiwa kwa historia ya jamii yote au ya sehemu ya jamii katika muktadha wa ulimwengu. Tunatumia nguvu ya ndani ya makavazi kwa uwezo wake wa kujenga ujasiri, kuongeza uelewa na kughihirisha simulizi zilizopo kwa pamoja, kupunguza migogoro ndani na kati ya vikundi na kuongeza uwezo wa amani endelevu.
Mtandao wetu unatoa fursa ya muunganiko na kutengeneza uelewa wa pamoja, kutoka maeneo mbalimbali ya kisiasa na kijiografia ambayo mara nyingi hayawezi kushirikishana kimawazo na uzoefu wa moja kwa moja. Kila mmoja akiwakilisha hoja mbadala kuhusu wakati ujao: Mgogoro wa mashariki ya kati, utatuzi wa muda mrefu wa migogoro ya baada ya vita na ukoloni wa ulaya kwa Africa. Makavazi yana nguvu ya kipekee katika nyakati hizi. Tunachambua kazi za makavazi na kuonyesha njia bora/nzuri/muafaka ya uhifadhi nyaraka/kumbukumbu kwa wakati ujao kwa lengo la kuendeleza na sio kukandamiza, ili jamii iwe na umoja na amani. Uharaka wa njia hii mpya unatokana na hali ya Mashariki ya Kati, na unalenga kushawishi kusaidia na kuendeleza mbinu zinazotokana na utatuzi wa migogoro baada ya vita Africa.

Katika kipindi hiki cha ujenzi wa baada ya vita unaofadhiliwa kwa mabilioni ya misaada ya kigeni ($1.2b kwa Syria), katika kusaidia kurejesha utulivu na amani, hapo ndipo umuhimu wa mradi wetu unaonekana. Mipango mikakati umesaidia kukua sana kwa miji (kutoka asilimia 50 hadi asilimia 80 huko Syria), uboreshaji huu ukipendelea sehemu ndogo ya jamii, kwa faida na gharama ya jamii husika na bila kulenga sehemu muhimu za kiutamaduni. Juhudi na miradi mizuri inaweza kuwa chanzo cha uvunjivu wa amani kwa kuvunja au kukata viungo muhimu vya jamii na utamaduni wao. Unyeti huu unachangia Zaidi uharibifu, mtawanyiko na ongezeko la mgawanyo wa kitabaka. Inaondoa pia faida ya mamilioni ya wanaoishi kwa shida, kama wakimbizi na wanaotafuta hifadhi katika makambi mengi ya wakimbizi.

Lengo letu ni kuwezesha kufungua na kutumia kwa umakini makavazi yaliyopo katika kutengeza makavazi mpya na kuweka mbinu za uhifadhi wa pamoja unaojali masimulizi mbalimbali. Mbinu na makavazi haya yatahifadhiwa katika maabara nne za kiuchunguzi zitakazokuwa Lebanon, Ghana, na Tanzania hii ni pamoja na shughuli muhimu zaidi za maabara kama vile miradi mbalimbali itakayoibuliwa. Katika kupitia makavazi zilizopo, makavazi maalum/rasmi na makavazi zisizo rasmi, zana za kisanaa za kidigitali, matukio ya wazi na jamii mbalimbali, lengo letu ni kuandaa kwa pamoja sera kwa mazungumzo ya pamoja na uongozi wa vyombo kama ICCROM. Nia yetu mtambuka katika kuonyesha tamaduni kama sehemu muhimu za majadiliano ni kusaidia utamaduni utambuliwe kama haki ya msingi ya kibinadamu.