Tunapofanya kazi

Michoro ya kisanaa—Abasia ya Wabenediktini; Ndanda, Tanzania 2019.

Tangu mwanzo, Tafakari Upya imeundwa na kuandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja. Katika msingi wake, tunalenga kuleta mabadiliko yanayo/yatakayochangia katika jamii kwa ujumla na amani endelevu kwa kuanzisha mtandao wa ushirikiano sawa, ajenda tafakurishi za kiutafiti, na shughuli zinazotokana na jamii yenyewe. Mtandao hu una muunganiko wa taaluma na elimu isiyo ya kitaaluma itakayozalisha mihimili ya uhifadhi yaraka wa pamoja na upana wa mbinu za pamoja ni nguzo kuu za tafakari upya. Timu yetu kubwa inaweza kuoneka kuwa ni tofauti. Lakini kiuhalisia imetokana na uzoefu wa muda mrefu wa kushirikishana maarifa na ufanyaji kazi wa pamoja wa watafiti, na washirika wengine ndani na nje ya mtandao ambao wana, nia na imani ambavyo ni vya muhimu sana katika kuandaa na kutekeleza malengo ya mradi huu. Shughuli zote zimejitokeza kutokana na mahitaji ya jamii, zinafuata mbinu za jamii husika, zikiratibiwa na wataalamu wetu kutoka nchi husika, washirika na watafiti wasaidizi pamoja na mitandao yao. Kazi yetu inakutana eneo maalum la baada ya migogoro, ujenzi wa jamii mpya na utawanyaji wa watu, msisitizo wa utafiti wa kwenye maabara na utekelezaji wa miradi ya wazi, na maeneo ya wanufaika wetu, ambapo mradi unataka kuwa na matokea chanya hasa: Tanzania, Ghana, Lebanoni, Afrika ya Kusini na kama ikibidi, Syria (angalia waraka wa ODA). Hapa wadau wetu muhimu ni: a) Makundi mbalimbali ndani ya jamii inayotoka kwenye migogoro ya zamani na ya sasa. b) Jumuiya, jamii na mashirika katika muktadha wa kutelekezwa, c) Serikali na mashirika yake yanayojihusisha na watu walio katika maeneo ya migogoro. Uhifadhi wa makavazi kama sehemu ya kumbukumbu, turathi na utengenezaji wa maeneo umeunganishwa na mtaji wa kijamii na nguvu ya kisiasa. Mradi unatumia mahusiano haya kuimarisha faida na kuondoa madhara kwa kutumia faida ya uhifadhi nyaraka wa pamoja ili kuibua masimulizi mbalimbali na mbadala yanayohusisha, yakawaida na yanayopinga simulizi za ukandamizaji au za aina moja.

Tunatekeleza hili kwa kuandaa eneo linaloonekana na lisiloonekana kwa ajili ya mazungumzo ya wazi yanayoongeza ushiriki na kuchochea uhifadhi na umiliki wa nyaraka katika mapana yake. Makavazi hii inahusisha wadau kuweza kupata na kutumia makavazi yaliyofungwa, yaliyofifishwa au kufutwa pia uwezo wa uhifadhi binafsi, ambao utasaidiwa na shughuli zilizoandaliwa kwa pamoja, utaalamu na mafunzo. Tunataka pia watunga sera kuelewa/kufahamu umuhimu wa utunzaji makavazi na masimulizi yasiyo rasmi pamoja na mahusiano yake na nguvu jamii. Kazi zetu pamoja na miradi ya kamisheni zitatoa vitu, mbinu, kuonyesha mifano ya namna gani mbinu hizi zinaweza kuchangia kupunguza migogoro ndani na nje ya jamii na hivyo kuongeza uwezekano wa amani endelevu (SDG 11, 16). Hii itaelezwa kwa undani ndani ya andiko la uhifadhi wa pamoja, litakaloandaliwa na kusambazwa kwa wadau mbalimbali. Miongoni mwa hao wadau watakuwa wale wanaohusika na utungaji wa sera za uhifadhi na utengenezaji upya, kuhakikisha kwamba mikakati haitaharibu maarifa ya jamii ila kwa kushirikisha maarifa na uelewa wa jamii kuhusu ni kipi cha thamani, kinafanya kazi kwa kuangalia matakwa na uvumbuzi wa jamii. Muundo wetu unaotegemea uandaaji wa pamoja na mazungumzo ya muda mrefu, utasaidia kuruhusu, na kuongeza uwezekano wa matokeo imara na ya kudumu.

Kazi yetu inaungwa mkono na sera madhubuti ya maadili pamoja na sera ya uangalifu salama, sera ya usawa wa kijinsia, pamoja na mafunzo yanayosaidia ushauri na ushauri wa michakato ya kuripoti. Miundombinu ya mradi huo ni pamoja na uwekezaji katika mawasiliano na upatikanaji kupitia ufadhili wa safari, uwezo wa kutafsiri, jukwaa la wavuti (lenye blogi za sasisho na kuonyesha, angalia viambatisho vilivyowekwa), na fursa za kidigitali pamoja na uhifadhi sahihi na kushirikishana data. Hii itahakikisha fursa zilizopo ndani ya nchikuwa na maana kiulimwengu. Uwezekano mkubwa wa fursa kubwa utatokana na kazi yetu, kama linavyoonekana kwenye kazi yetu ya majaribio nchini Tanzania (tazama kiambatisho kilichowekwa), ambayo tulishirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Barua yao ya udhamini inatoa muhtasari wa maoni ya washiriki juu ya uwezekano wa mradi kuwa fursa za muda mrefu, juu ya uboreshaji wa kikanda, fursa maradufu kwa vijana na wanawake kupitia njia za ubunifu wa urithi na ufundishaji: “…Hata katika hatua hii ya mwanzo ya mradi, jamii imeguswa moja kwa moja na hivyo bila shaka yoyote tunaamini kwamba kufanya kazi kwa pamoja ….kutakuwa na matokeo ya kudumu kwa mkoa wa Lindi….kama ilivyoonyeshwa jinsi jamii ya Lindi ilivyoshiriki kikamilifu hasa vijana na wanawake Mkoa una matumaini makubwa kuwa mradi huu umefika kwa wakati unaofaa .. Ushirikiano huu utachangia ufunguzi mpya wa ukanda wa kusini ambao hapo awali ulikuwa kitovu…na kufanya kama kiungo cha mazungumzo na kushirikishana maarifa….udigitishaji wa urithi wetu unaoonekana na usioonekana na usambazaji wake mashuleni tunaamini utakuwa na mafanikio na msaada mzuri na nyenzo ya kufundishia kwa kizazi kijacho. ”

Kupitia maabara na Tume maalum za kila nchi tutatengeneza njia za kuelekea fursa anuwai. Matokeo na faida zitatokana na: Kuanzisha uelewa wa pamoja wa kuhifadhi kumbukumbu kwa njia zinazohusiana; kuunda zana za kutekeleza na kutathmini utumiaji wake; kuandaa matokeo juu ya uwezo wake wa kuongeza mshikamano,ushirikishwaji, ukuaji na mwishowe kuzuia-mzozo. Faida za shughuli hii zitakuwa: Kuongezeka kwa mwamko; kukuwa kwa maarifa ya pamoja; kuongezeka kwa maswali muhimu ya utafiti ndani ya mtandao; kushirikiana na jamii; fursa zilizoimarishwa za mabadiliko katika mitizamo na tabia kupitia uundaji wa nafasi za mazungumzo na majadiliano; kujenga uwezo wa ndani na kuingiza maarifa na mitazamo ya ndani kuhusu makumbusho ya kitaifa na kimataifa. Matokeo na faida zinazotarajiwa kutokana na maabara hizi ni (matokeo na faida hizi ni tofauti na zile za kitaalam zilizoorodheshwa katika sehemu nyingine za maombi ya mradi):

Maabara ya 1: Tanzania

A) Filamu juu ya Vita ya Majimaji inayoonyesha kile kinachokumbukwa Pamoja na mitazamo ya walioathirika pamoja na vizazi vyao, ikiwaruhusu kuelezea historia na hadithi yao wenyewe. Filamu hiyo itaandaliwa Na kusambazwa na kutumika itakavyofaa katika taasisi za kitamaduni na kielimu; B) Nyenzo za kufundishia ni kwa maandishi sauti-na kuona, ikijumuisha hadithi mbalimbali na ubunifu wa watumiaji mwenyewe, kuimarisha njia za kujifunza historia zaidi ya simulizi moja iliyozoeleka; C) Ushirikiano wa kuongeza uwezekano wa ufikiaji na upatikanaji wa kumbukumbu katika makavazi ya Ndanda na Peramiho. Udigitishaji wa nyaraka zitakazowezekanika, na kwa kufuata maadili na taratibu ziweze kupatika bure mtandaoni. D) Uanzishaji wa eneo la kihistoria na kituo cha Utamaduni na kumbukumbu ya baadaye kwa kushirikiana na mkoa wa Lindi (ambao unaweza kuwa mwenyeji wa maonyesho ya mradi kwa mfano kutokana na ushirikiano na maabara ya 2 ya Baddawi. E) Ubunifu kutoka kwa michakato ya kuhifadhi kumbukumbu na uanzishaji kumbukumbu za kudumu zilizoundwa kwa ajili yao zinazofanya kazi na LDRC.

Maabara ya 2: Kambi ya Baddawi

Maabara hii, itashirikiana na maabara ya Tanzania na kujadili mambo matatu, itatumia uchunguzi wa pamoja wa mazingira ya uchungu/maumivu, usalama halisi/dhahiri na makazi yao, na uhusiano wa kihistoria wa Lebanon na Afrika, kutekeleza malengo ya mradi, kupitia: A) Maonyesho ya matukio mbalimbali kwa njia ya picha kutoka Tanzania. Haya yataonyewshwa katika kambi ya Baddawi, pia mahusiano kati ya gereza na makazi yaliyoshambuliwa. B) Uanzishaji wa maeneo ya kumbukumbu, makazi ya yaliyoshambuliwa ya PLO. C) Matokeo ya uhifadhi kumbukumbu wa pamoja, semina, picha, vipindi vya kidigitali na uandishi utategemea kile kinachoonekana kuwa kinafaa na kuhitajika. Tayari majaribio ya mradi yametoa maandishi ya ubunifu na mitazamo mipya kwenye maeneo ya kumbukumbu Kambini (Qasmiyeh 2019).

Maabara ya 3: Ghana

Matokeo ya shughuli za Maabara yatakuwa A) matokeo yatakusanywa na kusambazwa kwa kutumia njia ya mazungumzo, mikusanyiko ya watu, maonyesho ya picha za mnato, video na za kidijiti, mitandao ya kijamii, redio na vipindi vya runinga. B) Matokeo yatajumuish vipindi vya majadiliano juu ya usimamizi wa migogoro na uletaji wa amani, hii itatekelezwa kwa kushirikiana na Televisheni 3, 3-FM, Televisheni ya Ghana, Redio ya GBC na Televisheni ya Afrika. C) Kuandaa utunzaji wa data wa njia ya kidijiti inayoweza kufikiwa na mtu yeyote metadata hii ihusu tafiti muhimu pamoja na LDRC. Tutafanya kazi pia kwa karibu ilikuwezesha maabara ya Tanzania na washirika wote wa mradi kuwasilishwa kwa njia za kidigitali. D) Kuanzisha upya / kuamsha maeneo na hadithi, ambazo kupitia njia ya kuoanisha maeneo mabalimbali ya mradi itaruhusu jamii kutambua aina nyingi za masimulizi ya watu wa ukanda wa pwani na msimamo wao katika muktadha mpana wa ulimwengu.

Maabara ya 4: Beirut

Maabara hii inaazimia kupitia tena kwa umakini dhana ya jiji kama nyara. Hii italeta matokeo yafuatayo: A) Mpangokazi uliotengenezwa/Tafutwa na kukusanywa, kurekodiwa na kufikiriwa upya na kuandaliwa kama maeneo yaliyotumika na wadau mbalimbali. Hii itafanyika kwa kupitia; B) ziara, maonyesho, uigizaji na kurekodi, ili kuwezesha ufikiaji au upatikanaji mpana wa taarifa na uenezi wa uhamasishaji wa umma, kando na ukusanyaji na usambazaji wa taarifa na simulizi ambazo hazijahifadhiwa; C) Hatua ambazo zinafungua sehemu za jiji kuangazia simulizi za mseto kupitia michakato mingi ya kumbukumbu na kukuza mawazo ya baadaye katika sekta tofauti za wakaazi wa jiji na mamlaka.